1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MONROVIA:Maandamano ya ghasia usiku kucha mjini

19 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBOd

Vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa mataifa vilivyojihami kwa silaha wanashika doria katika barabara za mji mkuu wa Liberia baada ya wanajeshi waliorejea katika maisha ya kawaida kufanya maandamano ya ghasia usiku kucha.Vikosi hivyo vinashirikiana na polisi wa Liberia pamoja na wa Umoja wa mataifa.

Kulingana na walioshuhudia maandamano hayo mamia ya wanajeshi wa zamani wa Liberia,polisi,majeshi maalum ya usalama aidha maafisa wa uhamiaji waliandamana mjini ili kudai malipo ya marupurupu yao.

Waandamanaji hao waliweka vizuizi kwenye barabara za mji kwa kutumia mawe,magogo aidha kuwasha moto jambo lililoathiri usafiri.Polisi wa Liberia walioungwa mkono na polisi wa Umoja wa mataifa na jeshi lake walitawanya waandamanaji hao na kuwakamata watatu pekee.