MOGADISHU:Waislamu watangaza Jihad dhidi ya Ehtiopia nchini Somalia | Habari za Ulimwengu | DW | 10.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MOGADISHU:Waislamu watangaza Jihad dhidi ya Ehtiopia nchini Somalia

Kiongozi wa mabaraza ya kiislamu nchini Somalia sheikh Sharif Ahmed ametangaza vita vya jihad dhidi ya Ethiopia.Bwana Ahmed ametoa mwito huo mjini Magadishu alipokuwa anazungumza na wandishi habari. Tangazo hilo la vita limetolewa baada ya maafisa na watu walioshuhudia kusema kwamba wanajeshi wa serikali ya Somalia wakisaidiwa na majeshi ya Ethiopia waliuteka kwa muda mji wa Burahakaba uliopo kilometa 60 kusini mashariki ya mji wa Baidou kabla ya kuuachia na kurudi nyuma.

Lakini msemaji wa serikali ya Somalia amekanusha madai kuwa askari wa Ethiopia walishiriki katika kuuteka mji huo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com