1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU:Wadai kuhusika na jaribio la mauaji

5 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBui

Kundi la wanamgambo wa kiislam nchin Somalia limedai kuhusika na jaribio la kutaka kumuua Waziri Mkuu wa nchi hiyo Ali Mohamed Gedi hapo siku Jumapili ambapo walinzi sita wa kiongozi huyo waliuawa.

Mtu wa kujitoa mhanga alijilipua katika nyumba ya waziri mkuu huyo, likiwa ni jaribio la nne la kutaka kumuua waziri mkuu huyo.

Marekani imelilaani shambulio hilo na kusema mahafidhina hawatafanikiwa.

Msemaji wa Idara ya Usalama ya Marekani, Sean McCormack amesema Marekani itaendelea kutoa msaada kwa serikali ya mpito ya Somalia.

Wakati huo huo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban-Ki-Moon amemtuma mshauri wake wa juu wa masuala ya kisiasa kwenda Afrika Mashariki kwa mashariano ya jinsi ya kushughulikia mzozo nchini humo.

Afisa huyo Lynn Pascoe anatarajiwa kutembelea nchi kadhaa akianzia na Kenya.

Akiwa njiani atasimama mjini London kuhudhuria mkutano wa maafisa wa kundi la nchi zinazoshughulikia mzozo wa Somalia.