1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU:Wababe wa kivita waachia huru mateka, huku serikali ikiwanyooshea mkono wa amani

27 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCF4

Koo kubwa ya kikabila ya Hawiye huko Somalia hapo jana imewaachia huru askari 18 wa jeshi la serikali ya mpito ya Somalia, kufuatia maridhiano kati ya pande hizo mbili ya kuurejesha mji mkuu Mogadishu katika hali ya amani.

Askari hao walitekwa na wanamgambo wa kisomali wiki iliyopita katika siku mbili za mapigano makali yaliyoshuhudia watu 24 wakiuawa.

Wakuu wa Hawiye hapo siku ya Ijumaa walifikia makubaliano na majeshi ya Ethiopea yanayoisaidia Serikali ya Somalia, kusitisha mapigano.

Kiasi cha askari 26 wa Serikali inaarifiwa walitekwa katika mapigano hayo, ambapo ukoo wa Hawiye umekataa kuelezea wapi wanapowashikilia matekao hao, lakini taarifa zinasema kuwa huenda wako kusini mwa Mogadishu.

Wakati huo huo, Serikali ya Somalia imesema kuwa inataka kuwa mazungumzo ya maridhiano na ukoo huo mkubwa wa Hawiye.Wanamgambo wengi wakiislam wanatoka katika ukoo huo.

Waziri wa Ndani wa Serikali ya mpito ya Somalia, Muhamoud Hamed Gulled, amesema kuwa Serikali hiyo hivi sasa inafungua mlango wa kuwa na mazungumzo na wakuu wa ukoo huo.

Katika hatua nyingine, shirika la waandishi wa habari wasiyo na mipaka, limesema kuwa mwandishi wa habari wa radio ya Shabelle ya mjini Mogadishu pamoja na dereva wake ambao walikamatwa na serikali wameachiwa.