MOGADISHU:Rais wa Somalia ashikilia mkutano wa amani kufanyika | Habari za Ulimwengu | DW | 12.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MOGADISHU:Rais wa Somalia ashikilia mkutano wa amani kufanyika

Rais wa Somalia Abdullahi Yusuf Gedi anasisitiza kuwa mkutano wa maridhiano ya kitaifa unaotarajiwa kuanza katika siku tatu zijazo unaendelea bila mabadiliko yoyote.Kauli hiyo inatolewa kufuatia kuzuka upya kwa ghasia mjini Mogadishu zilizosababisha vifo vya yapata watu wanne.Makao ya rais yameshambuliwa katika ghasia hizo.Makombora kadhaa yalishambulia makao ya rais jana jioni huku moja lililoanguka katika eneo la Fiyore lililo karibu lilisababisha kifo cha mtu mmoja na kujeruhi wengine wawili.

Kwa mujibu wa afisa wa usalama wa serikali Mohammed Ganey aliyekuwamo ndani ya makao hayo ya rais,hakuna kombora lolote lililogonga majengo yoyote.

Watu wengine watatu waliuawa wakati ghasia zilipozuka katika maeneo kadhaa ya kusini mjini Mogadishu.Ghasia hizo zinatokea siku tatu kabla mkutano wa kujadilia amani kuanza.Mkutano huo umeahirishwa mara kadhaa.Wapiganaji wa kiislamu na majeshi ya serikali yamekuwa yakishambuliana tangu kufurshwa mapema mwaka huu na majeshi ya serikali yaliyoungwa mkono na majeshi ya Ethiopia.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com