1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mogadishu.Mapigano yasita, na wakaazi waanza kurejea.

27 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC6W

Mapigano yamesita na hakukuwa na milio ya makombora wakati wakaazi wa mji mkuu wa Somalia, Mogadishu wakitoa hisia tofauti leo kutokana na madai ya serikali ya ushindi baada ya siku tisa za mapigano makali dhidi ya wapiganaji wa Kiislamu. Haikufahamika wazi ni muda gani hali hiyo ya amani itaendelea wakati baadhi ya wakaazi wanarejea taratibu majumbani mwao.

Mitaa mingi ya mji huo haina watu, na hakuna wapiganaji kutoka pande zote walioonekana.

Mkaazi mmoja ambaye ni mwalimu wa shule ya sekondari Ahmed Warsame amesema kuwa watu wanahofia kurejea katika majumba yao kwa kuwa majeshi ya serikali na yale ya Ethiopia yameweka vizuizi barabarani katika baadhi ya maeneo ya mji huo.