1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mogadishu:Mamia ya familia zakimbia kuto Mogadishu kutokana na mapigano.

28 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7C2

Mamia ya familia zimekimbia kutoka mji wa Mogadishu hii leo kutokana na kuzuka upya mapigano baina ya waasi wa Kiislamu na majeshi ya usalama ya nchi hiyo yakisaidiwa na yale ya Ethiopia. Watu wanaonekana katika mitaa wakipakia mizigo katika malori na katika magari yanayovutwa na punda. Mashahidi wanasema si chini ya watu 10 wameuliwa pale majeshi ya Ethiopia yalipofanya mashambulio.