1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU:Makao ya rais yashambuliwa na makombora

12 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBjY

Yapata watu wane wamepoteza maisha yao katika ghasia zilizozuka upya mjini Mogadishu.Makao ya rais yameshambuliwa katika ghasia hizo mpya ikiwa ni siku chache kabla mkutano wa kujadilia amani kuanza mjini humo.

Makombora kadhaa yalishambulia makao ya rais jana jioni huku moja lililoanguka katika eneo la Fiyore lililo karibu lilisababisha kifo cha mtu mmoja na kujeruhi wengine wawili.

Kwa mujibu wa afisa wa usalama wa serikali Mohammed Ganey aliyekuwamo ndani ya makao hayo ya rais,hakuna kombora lolote lililogonga majengo yoyote.

Watu wengine watatu waliuawa wakati ghasia zilipozuka katika maeneo kadhaa ya kusini mjini Mogadishu.Ghasia hizo zinatokea siku tatu kabla mkutano wa kujadilia amani kuanza.Mkutano huo umeahirishwa mara kadhaa.Wapiganaji wa kiislamu na majeshi ya serikali yamekuwa yakishambuliana tangu kufurshwa mapema mwaka huu na majeshi ya serikali yaliyoungwa mkono na majeshi ya Ethiopia.