1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU:Hali ya usalama haijarudi kwenye mji mkuu wa Somalia

10 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBkN

Polisi nchini Somalia imesema wanajeshi wane wa serikali ya mpito ni miongoni mwa watu 13 waliouwawa katika mfululizo wa mashambulio ya mwishoni mwa juma mjini Mogadishu.Wanajeshi hao waliuwawa baada ya gari lao kukanyaga bomu la kufukiwa chini ya ardhi kaskazini mwa wilaya ya Huriwa.

Raia wengine wane waliuwawa kwenye soko la Bakara na wengine wane walipigwa risasi wakisubiri usafiri.

Mashambulio hayo yanadaiwa kufanywa na wapiganaji wakiislamu pamoja na watu wenye silaha wanaoipinga serikali.Kamishna wa polisi mjini Mogadishu Ali Said amethibitisha mashambulio hayo na amesema polisi inafanya opresheni ya kuleta amani katika mji mkuu Mogadishu.