MOGADISHU: Waziri mkuu wa mpito anusurika kifo | Habari za Ulimwengu | DW | 04.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MOGADISHU: Waziri mkuu wa mpito anusurika kifo

Waziri mkuu wa mpito wa Somalia Ali Mohamed Gedi amenusurika kifo baada ya gari lililokuwa na bomu kulipuka nje ya makaazi yake mjini Mogadishu.

Watu saba wameuwawa kufutaia shambulio hilo kati yao wakiwa ni walinzi watano wa bwana Ali Mohamed Gedi na raia wawili.

Bwana Gedi ambae alinusuriwa na wanajeshi wa kikosi cha kulinda amani cha umoja wa nchi za Afrika AU amewalaumu washambuliaji hao ambao anawatuhumu kuhusiana na kundi la kigaidi la Al Qaeda.

Shambulio hilo la jana jumapili limefuatia taarifa zilizosema kuwa manowari ya kivita ya Marekani ililenga makombora dhidi ya kundi linaloshukiwa kuwa ni la Al Qaeda katika milima ya kaskazini mwa Somalia katika jimbo linalojitawala kwa kadiri la Puntland.

Wakati huo huo maharamia wa kisomali wameiteka nyara meli ya shehena ya shirika moja la meli la Denmark.

Donica White iliyokuwa imesheheni vifaa vya ujenzi kutoka Dubai kuelekea Mombasa Kenya imetekewa nyara pamoja na mabaharia wake kilomita 120 katika pwani ya Somalia, maharamia hao pia wanazishikilia mashua tatu za uvuvi kutoka Taiwan na Tanzania pamoja na mashua nyingine ya India.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com