1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU: Watu takriban sita wauwawa

12 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCbK

Watu wasiopungua sita wameuwawa leo nje ya ikulu ya rais nchini Somalia. Watu hao wameuwawa wakati wa mapigano makali yaliyozuka kati ya walinzi wa rais na wanamgambo wa muungano wa mahakama za kiislamu.

Grenedi lilivurumishwa wakati wa machafuko hayo yaliyosababishwa na ugomvi wa mahala pa kuezeka gari la jeshi.

Mapigano hayo yamefanyika wakati wababe wa kivita walipokuwa wakifanya mazungumzo na rais wa serikali ya mpito ya Somalia Mohamed Abudalhi Yusuf mjini Mogadishu.

Wababe saba wa kivita wamekubali kuwapokonya silaha wapiganaji wao na kujiunga na serikali katika mazungumzo yao waliyokuwa nayo na rais Yusuf.

Wababe wa kivita na rais Yusuf wamerejea mjini humo baada ya wanamgambo wa kiislamu waliokuwa wakiudhibiti mji huo kufurushwa na majeshi ya serikali yakisaidiwa na majeshi ya Ethiopia.