MOGADISHU: Wapiganaji wa mahakama za kiislamu wawashambulia wanajeshi wa Ethiopia | Habari za Ulimwengu | DW | 20.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MOGADISHU: Wapiganaji wa mahakama za kiislamu wawashambulia wanajeshi wa Ethiopia

Wapiganaji wa mahakama za kiislamu nchini Somalia wamefanya shambulio la kuvizia msafara wa magari ya kijeshi ya Ethiopia na kuwauawa wanajeshi 6 na kuwajeruhi wengine 20. Wapiganaji wa mahakama za kiislamu ambao wanaidhibiti sehemu kubwa ya eneo la kusini mwa Somalia ukiwemo mji mkuu Mogadishu, walitishia kuyashambulia majeshi ya Ethiopia, wakati wote hao wakiwania udhibiti wa nchi. Ethiopia ilikanusha kuwa na maelfu ya wanajeshi nchini Somalia lakini ilikiri kuwa iliwatuma wataalamu wa kijeshi kuisaidia serikali dhaifu ya mpito yenye makao yake mjini Baidoa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com