MOGADISHU: Wanamgambo waapa kuanzisha vita vya chini kwa chini | Habari za Ulimwengu | DW | 06.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MOGADISHU: Wanamgambo waapa kuanzisha vita vya chini kwa chini

Kombora limerushwa karibu ya makao rasmi ya rais wa Somalia mjini Mogadishu.Mji wa Mogadishu umekabiliwa na wimbi la mashambulio,tangu wanamgambo wa Kiislamu kutimuliwa kutoka mji mkuu na vikosi vya Somalia vilivyosaidiwa na majeshi ya Ethiopia,mwishoni mwa mwezi wa Desemba.Kwa mujibu wa Marekani iliyokuwa ikiiunga mkono serikali dhaifu ya Somalia,inasemekana kuwa baadhi ya wanamgambo wa Kiislamu waliotimuliwa sasa wanajikusanya upya nchini Yemen na Saudi Arabia.Shambulio la hii leo,linadhihirisha hali mbaya ya usalama iliyopo mjini Mogadishu,siku chache baada ya wanamgambo kuapa kuwa wataanzisha vita vya chini kwa chini,dhidi ya serikali ya Somalia na wasaidizi wake wa Kiethiopia.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com