1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU: Umoja wa Afrika waidhinisha kikosi cha wanajeshi cha kulinda amani Somalia.

20 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCZT

Umoja wa Afrika umeidhinisha mpango wa kupeleka kikosi cha majeshi ya kulinda amani nchini Somalia ili kurejesha utangamano nchini humo.

Afisa mkuu wa Umoja huo amesema kikosi hicho kitapelekwa nchini humo kwa muda wa miezi sita na hatimaye kitasimamiwa na Umoja wa Mataifa.

Wanajeshi hao watachukua nafasi ya wanajeshi wa Ethiopia waliokwenda nchini humo mwezi uliopita kuisaidia serikali ya mpito kuwafurusha wanamgambo wa Kiislamu.

Mpango huo wa Umoja wa Afrika umetangazwa huku mapigano mapya yakiarifiwa yamezuka mjini Mogadishu.

Watu wasiojulikana walirusha kombora kwenye makao ya rais wa muda wa Somalia, Abdullahi Yusuf.