Mogadishu. Mwandishi mwingine auwawa. | Habari za Ulimwengu | DW | 25.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Mogadishu. Mwandishi mwingine auwawa.

Watu wenye silaha wamempiga risasi na kumuua mwandishi habari wa radio nchini Somalia jana Ijumaa, ikiwa ni mwandishi habari wa tatu kuuwawa katika muda wa wiki mbili.

Abdulkadir Mahad Moallim Kaskey , aliyekuwa akifanyakazi katika radio Banadir, aliuwawa wakati watu wenye silaha walipofyatua risasi dhidi ya basi dogo kusini magharibi ya jimbo la Gedo.

Abiria mwingine alipata majeraha katika shambulio hilo lililofanyika wakati wa asubuhi. Watu waliofanya shambulio hilo bado hawajulikani. Shambulio hilo la Ijumaa linafanya idadi ya waandishi habari waliouwawa hadi sasa kufikia saba mwaka huu.

Wakati huo huo watu wanane wameuwawa katika mapigano yaliyotokea wakati wa usiku nchini Somalia kati ya majeshi ya serikali na waasi. Majeshi ya Somalia yamewauwa waasi saba na kupoteza mwanajeshi mmoja katika mapigano yaliyotokea siku ya Alhamis.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com