MOGADISHU : Mashambulizi ya mizinga yauwa watu kadhaa | Habari za Ulimwengu | DW | 11.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MOGADISHU : Mashambulizi ya mizinga yauwa watu kadhaa

Takriban watu wanane wameuwawa na wengine kadhaa kujeruhiwa hapo jana katika mashambulizi ya mizinga na magurunedi kwenye mji mkuu wa Somalia Mogadishu katika kile kinachonekana kama kupamba moto kwa mashambulizi ya wapiganaji wa chini kwa chini.

Masaa machache baadae kambi iliokuwa na wanajeshi wa Ethiopia kusini mwa Mogadishu ilikuja kushambuliwa vikali. Mabomu kadhaa yalivurumishwa kwa mizinga katika soko lililofurika watu kusini mwa mji mkuu huo na kuuwa watu watatu na kujeruhi wengine kadhaa.Watoto wawili pia wameuwawa wakati mabomu yalipoangukia kwenye kambi ya watu waliopoteza makaazi yao.

Maafa mengine yametokea kutokana na mashambulizi ya mizinga na magurunedi katika sehemu zilizo karibu na ofisi za Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP na uwanja wa ndege wa kimataifa pamoja na kitongoji cha Gupta.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com