Mogadishu. Mapigano yazuka tena. | Habari za Ulimwengu | DW | 08.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Mogadishu. Mapigano yazuka tena.

Wanamgambo wa Kiislamu wanapambana na majeshi ya Ethiopia katika mji mmoja kusini mwa Somalia, afisa mmoja wa ngazi ya juu wa kundi hilo la Waislamu amesema leo. Hii itakuwa ni mara ya kwa wanamgambo hao wa Kiislamu ambao wanadhibiti eneo kubwa la kusini mwa nchi hiyo kupigana ana kwa ana na majeshi ya Ethiopia.

Wakati huo huo makundi hasimu ya kivita yamekuwa yakipigana leo katikati ya Somalia, na kuongeza hali ya wasi wasi kuwa kunaweza kutokea vita kamili siku mbili baada ya umoja wa mataifa kuidhinisha uwekaji wa majeshi ya kulinda amani nchini humo.

Kuhusiana na majadiliano ya amani baina ya serikali mjini Baidoa na kundi la muungano wa mahakama za Kiislamu linaloshikilia mji mkuu Mogadishu , balozi wa Somalia katika umoja wa mataifa Idd Bedel Mohammed amesema serikali ya nchi hiyo iko tayari kufanya majadiliano lakini kwa masharti.

O-Ton Mohammed.

Wapiganaji wa Kiislamu wamesema kuwa wameshambuliwa katika kituo chao mjini Bandiradley, kiasi cha kilometa 630 kaskazini ya Mogadishu na wanamgambo wanaoungwa mkono na serikali na wakisaidiwa na majeshi ya Ethiopia na kuzusha mapigano hayo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com