Mogadishu. Mapigano yazuka tena kwa muda. | Habari za Ulimwengu | DW | 05.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Mogadishu. Mapigano yazuka tena kwa muda.

Mapigano makali yamezuka tena kwa muda mfupi usiku katika wilaya moja mjini Mogadishu ambako majeshi ya Ethiopia yanapambana na wapiganaji wa Kiislamu na wapiganaji wa Kiukoo.

Maeneo mengine ya mji huo yalibaki kuwa shwari kwa muda wa siku nne sasa, wiki moja baada ya kuzuka kwa mapigano makali katika mji huo ulioharibiwa kwa vita katika muda wa miaka 15.

Majeshi ya Ethiopia yanashika doria ndani na nje ya uwanja mkuu wa mpira na yamekuwa yakipambana na wapiganaji, waliojipanga katika mitaa ya eneo hilo tangu mapigano yalipozuka siku ya Jumapili.

Wakaazi wengi wamekimbia eneo hilo, pamoja na eneo jirani la Al Kamin , eneo ambalo lilikuwa na mapigano makali yaliyozuka siku ya Alhamis wiki iliyopita.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com