Mogadishu. Mapigano bado yanaendelea. | Habari za Ulimwengu | DW | 23.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Mogadishu. Mapigano bado yanaendelea.

Mapigano yanasemekana kuwa yanaendelea kati ya majeshi yanayounga mkono umoja wa mahakama za Kiislamu na majeshi ya serikali dhaifu ya mpito ya nchi hiyo.

Pia kuna ripoti kuwa Ethiopia imetuma vifaru na helikopta katika mstari wa mbele wa mapambano kusaidia majeshi ya serikali ya Somalia.

Muungano wa mahakama za Kiislamu tayari wanadhibiti mji mkuu Mogadishu na maeneo makubwa ya taifa hilo la pembe ya Afrika.

Pande zote mbili zimetangaza kutoa kipigo kwa upande mwingine baada ya siku kadha za mapigano, lakini hakuna taarifa za kuthibitisha madai hayo.

Mashirika ya kutoa misaada yamesema kuwa raia wanakimbia mapigano hayo na wanasema kuwa wana wasi wasi kuhusu wafanyakazi wao walioko katika maeneo hayo, ambao wanafanyakazi kuwasaidia wahanga baada ya wiki kadha za mvua kubwa.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com