1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU: Maelfu ya raia wakimbia Mogadishu

11 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CBK2

Maelfu ya watu wanaukimbia mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, huku mapigano mabaya zaidi kuwahi kutokea mjini humo mwaka huu yakiendelea.

Idadi ya watu waliouwawa kwenye mapigano kati ya wanamgambo wa kiislamu na wanajeshi wa Ethiopia wanaoiunga mkono serikali ya mpito ya Somali inayolegalega imefikia 80.

Jana kulikuwa na utulivu mjini Mogadishu huku lakini kulikuwa na wasiwasi mkubwa miongoni mwa wakaazi wa mjini humo.

Madaktari wanasema wanapata shida kuwatibu majeruhi kwa sababu ya ukosefu wa dawa na vitanda vya kuwalaza wagonjwa hospitalini.