MODENA: mwanamuziki mashuhuri Luciano Pavaroti aaga dunia | Habari za Ulimwengu | DW | 06.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MODENA: mwanamuziki mashuhuri Luciano Pavaroti aaga dunia

Mwanamuzuiki mashuhuri wa mtindo wa Opera Luciano Pavaroti ameaga dunia leo nyumbani kwake katika mji wa Modena kaskazini mwa Italia.

Pavaroti alikuwa na umri wa miaka 71 na aliugua ugonjwa wa kansa ya kongosho.

Pavaroti alilemewa na maradhi tangu alipofanyiwa operesheni mwezi julai mwaka 2006 na tangu hapo hakuwahi tena kujitokeza hadharani hadi mauti yalipomkuta hii leo.

Muziki wake wa Opera uliwagusa takriban wapenzi bilioni 1.5 ulimwenguni.

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon ameuutambua mchango mkubwa wa marehemu Pavaroti kwa masikini kote duniani.

Waziri mkuu wa Italia Romano Prodi amesema nchi yake imepoteza sauti yenye miujiza.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com