Mo Farah ashinda dhahabu ya mita 10,000 | Michezo | DW | 22.08.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Mo Farah ashinda dhahabu ya mita 10,000

Katika matokeo mengine, Muingereza Mo Farah ametetea taji lake la ulimwengu katika mbio za mita 10,000 na kuendelea kutawala mbio hizo kwa upande wa wanaume katika mashindano makuu

Mkenya Geoffrey Kamworor alizidiwa kasi katika mita 100 za mwisho lakini akamaliza katika nafasi ya pili na kunyakua nishani ya fedha wakati mwenzake Paul Tanui akinyakua shaba katika nafasi ya tatu.

Farah mwenye umri wa miaka 32, ambaye ni bingwa wa sasa wa ulimwengu katika mbio za mita 5,000 na 10,000 sasa ameshinda mataji sita katika mbio hizo mfululizo katika mashindano makuu.

Mwandishi: Bruce Amani/reuters
Mhariri: Mohamed Dahman