1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

"Mmwisho wa enzi ya kimabavu hauko mbali " anasema Morgan Tsvangirai

18 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCHk

London:

Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Zimbabwe Morgan Tsvangirai,amesema “mzozo wa Zimbabwe umefikia kileleni”.Akihojiwa na kituo cha televisheni cha BBC hii leo,Morgan Tsvangirai amesema Zimbabwe haiko mbali na kujikomboa.Mkuu huyo wa chama cha MDC amesema tunanukuu:”Hali si nzuri lakini naamini mzozo unakurubia kilele chake na tutajionea mwisho wa enzi ya muimla” mwisho wa kumnukuu.Morgan Tsvangirai na wanaharakati zaidi ya 50 wengine wa upande wa upinzani walikamatwa mwishoni mwa wiki iliyopita na kupigwa vibaya sana kwa kushiriki katika maandamano dhidi ya utawala wa rais Robert Mugabe.Picha za viongozi waliovimba nyuso kwa kupigwa zimezusha lawama kali kote ulimwenguni.