Mmoja wa washukiwa wa utekaji nyara wa watotowa kiafrika atolewa mahakamani Chad akiwa hoi | Habari za Ulimwengu | DW | 24.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Mmoja wa washukiwa wa utekaji nyara wa watotowa kiafrika atolewa mahakamani Chad akiwa hoi

N’DJAMENA:

Muuguzi mmoja wa kifaransa,na wenzake watano wanaokabiliwa na kesi ya kuwateka nyara watoto 103 wa Kiafrika,ameondolewa mahakamni leo akiwa hoi baada ya kugomea chakula kwa mda mrefu.

Nadia Merimi pamoja na wenzake wengine watano wa shirika la misaada la Zoes Ark,mapema mwezi huu ,walianza mgomo wa kutokula kutokana na hali waliomo kwa sasa.

Watu sita wanadai kuwa walitaka kuwaokoa watoto maskini kutoka Sudan na kuwapeleka Ulaya.

Wendesha mashtaka wanasema watoto wote ni raia wa Chad waishio na familia zao.

Raia wengi wa Chad nao wanakabiliwa na kesi hiyo.Ikiwa watapatikana na hatia ,wafanya kazi hao wa kifaransa hawatatekeleza adhabu yao nchini Chad bali Ufaransa.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com