1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mlipuko katika mgodi wauawa kadhaa China

21 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CvQQ

BEIJING.

Mlipuko wa gezi katika mgodi usio kuwa halali kaskazini mwa china umewauwa watu wasiopungua 20.Shirika la habari la China Xinhua limesema jumatatu kuwa mlipuko ulitokea wakati wafanya kazi katika mgodi huo walipokuwa wanajaribu kufungua tena mgodi haramu katika mkoa wa Shanxi ambao ulifungwa na serikali ikitumia baruti mwaka wa 2004.

Migodi ya mkaa ya China ndio hatari kuliko yote duniani kwa kutokea mioto ya kila mara ,mafuriko pamoja na mikasa mingi mingineyo kila mwaka,licha ya ahadi ya kila mara ya serikali ya kuboresha hali.Wachimba migodi 3000 walikufa nchini China mwaka jana ambapo ni sawa na watu 10 kwa wastani wa kila siku.