1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mladic atolewa mahakamani

4 Julai 2011

Mkuu wa Zamani wa Jeshi la Waserbia wa Bosnia Ratcko Mladic ameondolewa mahakani katika ya UN ya uhalifu anaotuhumiwa kuutenda wakati wa vita vya Bosnia Herzgovina, kwa kubishana na jaji wa The Hague.

https://p.dw.com/p/11onc
Mkuu wa Zamani wa Jeshi la Waserbia wa Bosnia Ratcko MladicPicha: AP

Hatua hiyo inafuatia kitendo chake cha kukataa kujibu mashitaka na mara kwa mara utaratibu wa majaji mahakamani mjini The Hague.

Mladic anatuhumiwa kwa makosa 11 ya mauaji,uhalifu dhidi ya binaadamu na uhalifu wa kivita yanahusiana na vurugu za miezi 43 za katika maeneo ya mji mkuu wa Bosnia, Sarajevo.

Wakati wa kusilikiza mashitaka hayo Jaji Alphons Orie alishindwa kumvumila Mladic mwenye umri wa miaka 69, ambae alikuwa akiendelea kujiingiza kati mfululizo .

Kisa hicho kilimuondoa katika chumba cha mkutano, huku mtuhuwa huyo akilalamika kwa sauti ya juu kwa kuelekeza lawama zake kwa majaji watatu walikuwa wakisiliza kesi hiyo, akisema hawampi nafasi ya kupumua.

Kwanza Mladic alilalamika kuwa hawezi kusikia vitzuri jinsi kikao cha mahakama kinavyoendelea na baadae akadai kuwa anahisi baridi kichwani. Akamuuliza Jaji kama anaweza kuavaa kofia yake ambayo awali alitakiwa kuivua. Mladic akatamka kwa kelele " Nina baridi kichwani, niache nivae kofia yangu, ninapokuwa na baridi mwili wangu huawa hauafanyi akazi."

Jaji Orie alilikataa ombi hilo na kumuonya Jenerali huyo wazamani asizungumze na waliohudhuria badala yake azingatie katika kusikiliza mwenendo wa kesi inayomkabili.

Hata hivyo Mladic alionesha ukaidi, jambo ambalo lilimfanya Jaji amuonye kwamba endapo akiendelea kuzungumza na umma basi ataweza kumuondoa katika chumba cha mahakama.

Lakini baadae jaji alijaribu kuendele ambapo pia Mladic aliingilia mazungumzo yake ndipo ambapo ikaamuliwa maafisa usalama wa Umoja wa Mataifa mahakamani wamtoe nje ya mahakama.

Muda mfupi kabla ya kutekelezwa amri hiyo Mladic alimwambia Jaji Orie kwamba afanye chochote anachotaka kufanya, bila ya mwanasheria wake hana sababu ya kupokea chochote au kusema chochote.

Mkuu wa huyo wa majeshi ya Waserbia wa Bosnia aliwaambia majaji wa mahakama kwamba anamtaka wakili wake wa sasa aliomteua ambae anachukua nafasi ya mawakili wawili kutoka Belgrade.

Mladic alikamatwa Mei 26, huko Kaskazini mwa Serbia baada kusakwa kwa takribani mika 16, akasafirishwa hadi The Hague siku tano baadae na kupandishwa kizimbani mara ya kwanza tarehe 3 mwezi uliopita wa Juni.

Mwandishi Sudi Mnette/AFP

Mhariri: Abdul-Rahman, Mohammed