1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkuu wa zamani wa jeshi la Rwanda apigwa risasi

Prema Martin/DPA20 Juni 2010

Mkuu wa zamani wa jeshi la Rwanda, Faustin Kayumba Nyamwasa alipigwa risasi siku ya Jumamosi nje ya nyumba yake katika mji wa Johannesburg nchini Afrika Kusini.

https://p.dw.com/p/NxrS

Kwa mujibu wa msemaji wa polisi, Govidsamy Mariemutho, mtu asiejulikana alitoka kwenye gari na akampiga risasi tumboni Nyamwasa.Jemadari huyo alijeruhiwa vibaya na amepelekwa hospitali lakini maisha yake hayako hatarini.

Nyamawasa alikuwa akijulikana kama mkosoaji wa Rais wa Rwanda Paul Kagame na aliondoka Kigali pamoja na familia yake mwezi wa Februari. Mke wa Nyamwasa ameliambia shirika la habari la Afrika Kusini SAPA, kuwa anaamini shambulio hilo lilikuwa jaribio la kumuua mume wake.

Maafisa nchini Ufaransa na Uhispania wametoa waranti ya kumkamata Nyamwasa kwa madai ya kuhusika na mauaji ya kimbari yalioyotokea mwaka 1994 nchini Rwanda. Hadi watu 800,000 walipoteza maisha yao katika mauaji hayo.