Mkuu wa zamani wa jeshi la DRC akamatwa | Matukio ya Afrika | DW | 17.01.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Mkuu wa zamani wa jeshi la DRC akamatwa

Faustin Munene, ambaye ametuhumiwa  kupanga mapinduzi ya kijeshi dhidi ya rais Joseph Kabila mnamo mwaka 2011, amekamatwa nchini Gabon

Mkuu wa jeshi wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Faustin Munene, ambaye ametuhumiwa  kupanga mapinduzi ya kijeshi dhidi ya rais Joseph Kabila mnamo mwaka 2011, amekamatwa nchini Gabon. Taarifa ya chama kilichoasisiwa na Munene cha Convention of the People for Progress and Democracy (CPPD) imesema alikamatwa tokea Januari 10.

Afisa mmoja wa Gabon amethibitisha kwa kusema maelezo zaidi bado hayakuwekwa wazi, na haijulikani kama Jenerali Munene atarudishwa nyumbani DRC. Hata hivyo wizara za mambo ya ndani na nje za Gabon bado hazikuthibitisha kukamatwa huko.

Munene alikuwa waziri wa mambo ya ndani na mkuu wa vikosi vya jeshi la DRC chini ya uongozi wa baba yake rais Kabila, Laurent-Desire Kabila. Anashutumiwa kuhusika na mashambulizi ya Febuari 27 mwaka 2011 nyumbani kwa Kabila na katika kambi ya jeshi. Washambuliaji kumi na moja na wanajeshi wanane waliuawa.