1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkuu wa shirika la ujasusi la Brazil asimamishwa kazi kwa muda

2 Septemba 2008

-

https://p.dw.com/p/F90c

BRASILIA

Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva amemsimamisha kazi kwa muda kazi mkuu wa idara ya kijasusi nchini humo kufuatia kuhusika na kashfa ya kutega mawasiliano ya maafisa wa ngazi za juu akiwemo mwanasheria mkuu wa mahakama kuu.

Taarifa kutoka ofisi ya rais imesema kwamba mkuu huyo wa kijasusi Paulo Lacerda ameondolewa kwa muda kazini ili uchunguzi ufanyike.

Kashfa hiyo nzito imeibuka mwishoni mwa wiki hii baada ya gazeti moja la nchini humo Veja kuchapisha habari zilizodai kwamba mawasiliano ya maafisa wa juu akiwemo mwanasheria mkuu,wabunge na maafisa walio karibu na rais Da Silva yanategwa na shirika hilo la kijasusi.

Hii ni kashfa ya kwanza nzito katika kipindi cha miaka sita ya utawala war ais Lula Da Silva ulioingia madarakani kwa ahadi ya kuisafisha serikali.