1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Mataifa wataka kurejeshwa demokrasia Afrika

12 Septemba 2023

Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Turk leo ametoa mwito wa kurejeshwa haraka utawala wa kiraia kwenye mataifa ya Afrika yaliyoshuhudia mapinduzi ya kijeshi.

https://p.dw.com/p/4WCgm
Schweiz, Genf: Volker Türk, UN-Hochkommissar für Menschenrechte
Mkuu wa shirika la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa Volker TurkPicha: Salvatore Di Nolfi/KEYSTONE/dpa/picture alliance

Mkuu huyo wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa  Volker Turk amesema mwenendo wa kuchukua madaraka kwa nguvu siyo suluhu kwa matatizo yaliyopo.

Katika hotuba yake mbele ya mkutano wa majira ya mapukutiko wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, Volker amesema njia pekee kuyashughulikia matatizo ni kuwa na utawa kiraia unaotoa nafasi kwa umma kuwa huru kuikosoa serikali na kushinikiza mageuzi.

Amezungumzia pia athari za mabadiliko ya tabianchi na ukosefu wa huduma muhimu akisema ndiyo yanachangia  hali ya kukata tamaa miongoni mwa raia duniani na kuchochea hisia za itikadi kali. Hotuba hiyo ya jumla imemumilika vilevile mizozo ya wakimbizi tangu Myanmar, huko Mexico na hata nchini Mali.

Ukosefu wa usalama nchini Haiti na ukandamizaji wa makundi ya walio wachache  ulimwenguni ni sehemu ya masuala mengi yaliyoorodheshwa na mkuu huyo wa haki za binadamu kama changamto zinazoikabili dunia.