1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkuu wa CAF alaumu kufungwa lango katika mkasa wa AFCON

Bruce Amani
26 Januari 2022

Rais wa shirikisho la kandanda Afrika – CAF Patrice Motsepe amesema uamuzi « usioelezeka » wa kufunga lango la uwanja wa mpira ulisababisha mkanyagano uliowauwa watu wanane kabla ya mechi ya Kombe la Mataifa ya Afrika

https://p.dw.com/p/466NJ
Kamerun Africa Cup Pressekonferenz Patrice Motsepe
Picha: Muzi Ntombela/Sports Inc/empics/picture alliance

Rais wa shirikisho la kandanda Afrika – CAF Patrice Motsepe amesema uamuzi « usioelezeka » wa kufunga lango la uwanja wa mpira ulisababisha mkanyagano uliowauwa watu wanane kabla ya mechi ya Kombe la Mataifa ya Afrika katika mji mkuu wa Cameroon, Yaounde Jumatatu jioni.

« Lango hilo lilipaswa kuwa wazi kwa sababu kama lingekuwa wazi wangeweza kuingia, na kwa sababu sizizoelezeka likafungwa, » amesema rais huyo wa CAF katika kikao cha waandishi wa habari.

Mtoto ni miongoni mwa waliouawa, huku watu 38 wakijeruhiwa wakati mashabiki walijaribu kuingia katika dimba la Olembe ambako wenyeji Cameroon walikuwa wanacheza dhidi ya Comoro.

Motsepe ametoa wito wa uchunguzi baada ya Rais wa Cameroon Paul Biya awali kuamuru uchunguzi « ili kufahamu kilichosababisha mkasa huo. »

Mechi ya robo fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika iliyotarajiwa kuchezwa katika dimba la Olembe Jumapili itahamihiswa uwanja wa Ahmadou Ahidjo, pia mjini Yaounde. 

Afp