1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafadhili na wapokea misaada wakutana mjini Accra.

Duckstein, Stefanie (DW Afrika) 3 Septemba 2008

Wajumbe zaidi ya 1000 kutoka nchi wafadhili na wapokeaji misaada wanaendelea na mkutano wao mjini Accra-Ghana kujadili njia za kuimarisha ushirikiano wa maendeleo.

https://p.dw.com/p/FAXY
katikati , Waziri wa Ujerumani Heidemarie Wieczorek Zeul anaeshuhgulikia ushirikiano wa maendeleo.Picha: AP


Wajumbe zaidi  ya alfu moja  kutoka nchi wafadhili  na  zinazoendelea wanaendelea na mkutano wao mjini Accra- Ghana, kujadili  njia  za kuimarisha  ushirikiano wa  maendeleo. 


Wajumbe hao  wanajadili njia  za kuimarisha ushirikiano sambamba na kuhakikisha  uwajibikaji katika matumizi ya  misaada ya  maendeleo.  Wapinzani wanasema  misaada  inayotolewa  ni midogo  na  haina  ufanisi. kama anavyoeleza Mkurugenzi  wa  asasi  isiyo ya kiserikali nchini Kamerun Kuenzob anaehudhuria   mkutano  huo amesema kuwa katika kazi  zake za kila siku anashuhudia mashindano  baina ya wafadhili  wa kimataifa.

Malalamiko  kama  hayo yametolewa na wajumbe  kutoka Kenya,Afghanistan ,Pakistan na kutoka nchi nyingi zinazopokea  misaada ya maendeleo.

Njia  ya kutatua  tatizo hilo ni kuoanisha juhudi  za watoaji   na  wapokeaji misaada, ameeleza Ingrid Gabriela Hoven  kutoka wizara  ya ushirikiano wa uchumi nchini  Ujerumani. Kuhusu urudufu wa miradi, mjumbe huyo kutoka Ujerumani amesema  pana haja  ya kuzileta   pamoja juhudi  za wafadhili  wa kimataifa ili kuweza kuziratibisha.


Wajumbe  kutoka  nchi  zinazoendelea kwenye   mkutano huo wa  siku nne mjini Accra nao wamesisitiza  umuhimu wa kuzijumuisha  asasi za raia  katika miradi ya maendeleo. Watetezi wa hoja hiyo wanasema kuwa  asasi  hizo  ndizo zinazoleta  maendeleo na siyo serikali.