Mkutano wa UNCTAD wamalizika leo huko Accra,Ghana | Matukio ya Kisiasa | DW | 25.04.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Mkutano wa UNCTAD wamalizika leo huko Accra,Ghana

Afrika sio kikapu cha kuombea misaada, lakini bara hilo linaungulika tu kutokana na athari za visa na mikasa ambayo haliwezi kuidhibiti.

Mwenyekiti wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon kwenye mkutano wa UNCTAD huko Ghana

Mwenyekiti wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon kwenye mkutano wa UNCTAD huko Ghana

Hayo ni maneno ya mwanaharakati wa kutoka Togo, EKPLOM AFEKA, anayehudhuria mkutano wa 12 wa Shirika la Umoja wa Mataifa juu ya Biashara na Maendeleo, UNCTAD, unaofanyika mjini Accra, Ghana, tangu tarehe 20 mwezi huu hadi leo. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, katika mkutano huo pia alivunjwa moyo na majaribio madogo sana yanayofanywa na jamii ya kimataifa kuengeza biashara na uwezekaji katika Afrika.

Bibi Hamida Maalim, mhadhiri mwandamizi wa Chuo Kikuu huko Ghana, amehudhuria mkutano huo wa UNCTAD, akiwakilisha jumuiya isiokuwa ya kiserikali, na alimwambia Othman Miraji nini kile kilichoamuliwa katika mkutano huo wa Accra.

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com