1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa Umoja wa Ulaya, Brussels.

Halima Nyanza29 Oktoba 2010

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wamekubaliana kuyapitia mapendekezo yaliyotolewa na Ujerumani, juu ya mfumo wa kuzuia kutokea tena kwa msukosuko wa fedha.

https://p.dw.com/p/PrVl
Mstari wa mbele kushoto kuelekea kulia ni Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya Manuel Barroso, Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy, Rais wa Lithuania Dalia Grybauskaite na waziri mkuu wa Ubelgiji Yves Leterme. nyuma kutoka kushoto Waziri mkuu wa Slovenia Borut Pahor, Waziri mkuu wa Ureno Jose Socrates, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na Waziri mkuu wa Finland Mari Kiviniemi wakati wa picha katika mkutano wa EU mjini Brussels, Ubelgiji.Picha: AP

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wamekubaliana kuyaangalia kwa makini mapendekezo yaliyotolewa na Ujerumani, juu ya mfumo wa udhamini uliobuniwa kuzuia kutokea tena kwa msukosuko wa fedha, kama ule, uliotokea nchini Ugiriki mapema mwaka huu.

EU Gipfel in Brüssel Belgien
Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel.Picha: AP

Hayo yamesema leo asubihi na kansela wa Ujerumani Angela Merkel mjini Brussels, Ubelgiji kunakofanyika mkutano wa kilele wa viongozi wa Umoja wa Ulaya.

Wanachama wa Umoja wa Ulaya wataamua juu ya jambo hilo, ifikapo mwezi Desemba.

Lakini mpango wenye utata, uliotolewa na Ujerumani na Ufaransa juu ya kuzuia haki ya kupiga kura, mataifa wanachama ambayo yatavunja sheria za bajeti za umoja huo, umeendelea kukosolewa vikali.

Mapendekezo yote yatakayojadiliwa katika mkutano huo wa siku mbili mjini Brussels, yatahitaji kufanyiwa mabadiliko kwa mkataba wa Lisbon wa umoja huo.