Mkutano wa mawaziri wa G8 mjini Dresden | Matukio ya Kisiasa | DW | 09.05.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Mkutano wa mawaziri wa G8 mjini Dresden

Masilahi ya jamii yazingatiwe zaidi na viongozi wa mataifa tajiri kwa viwanda-wanasema mawaziri

Mawaziri wa kazi wa G8

Mawaziri wa kazi wa G8

“Kimsingi mkutano huo wa siku tatu ulizungumzia” hali ya raia wa kawaida”-kama anavyosema waziri wa kazi wa serikali kuu ya Ujerumani Franz Münterferimng wa kutoka chama cha Social Democratic SPD.Hata hivyo mkutano huo wa mawaziri wa mataifa sabaa tajiri kwa viwanda pamoja na Urusi-G8 haujawashughulisha watu sana.

Japo kama masuala yanayohusu kwa mfano ulimwengu unaozidi kujongeleana na utandawazi yamehanikiza,lakini yanafungamanishwa zaidi na faida na masoko ya hisa-na sio na masoko ya ajira.Hiyo ndio maana mawaziri wa G8 wanapanga siku za mbele kuyajongeza mbele zaidi masuala ya ajira na jamii katika utaratibu mzima wa utandawazi-hata kama maazimio na matarajio hayakua yakitegemewa kutangazwa katika mkutano huo wa mjini Dresden.

“Waraka wa mwisho” ndivyo ilivyoitwa taarifa iliyotangazwa jana mjini Dresden mkutano wa mawaziri wa nchi sabaa tajiri kwa viwanda na Urusi G8 ulipomalizika.Ndani ya waraka huo mawaziri hao wameelezea miito yao na nasaha kwa viongozi wa taifa na serikali watakaokutana wiki chache kutoka sasa katika mji wa mwambao wa Heiligendamm.Mwenyeji wa mkutano huo wa Dresden,waziri wa kazi wa serikali kuu ya Ujerumani Franz Münterfering ameyataja yale yalimo ndani ya waraka huo ambao yeye na wenzake wamewatumia viongo wa serikali za nchi zao.

“Tunakuombeni:zungumzieni pia kuhusu masuala yanayohusiana na jamii,mafungamano yaliyoko kati ya mazingira,uchumi na jamii.Ni muhimu kuleta wizani kati ya mada hizo.”Amesema bwana Münterfering.

“Utandawazi uzingatie mahitaji ya jamii”-ndio kauli mbiu ya mkutano huo-hasa kwa kutilia maanani jinsi ya kuinua kiwango cha maisha katika mataifa yanayoendelea na yale yanayaoinukia ili kuweza kukikurubia kiwango cha maisha cha mataifa manane tajiri kwa viwanda G8.

Waziri wa kazi wa serikali kuu ya Ujerumani Franz Münterfering anaendelea kusema:

„Kinga ya jamii,inamaanisha kuwaondolea hofu na maafa binaadam-kuhakikisha,mbali na kupata chakula na maji,wanajivunia pia hifadhi ya jamii wanapokua katika umri wa kustaafu.“

Waziri wa huduma za jamii wa Brazil Luis Marinho alialikwa kama mgeni wa heshima katika mkutano huo wa Dresden na alipangiwa kimsingi kuzungumzia juu ya mfumo wa malipo ya uzeeni nchini mwake.Mwanaharakati huyo wa zamani wa chama cha wafanyakazi hakuiacha bila ya shaka fursa ya kutilia mkazo kile anachoamini yeye kua ungekua utaratibu wa haki wa utandawazi ulimwenguni.Nchi zinazoendelea zinajitahidi kuchangia ipasavyo.Lakini nchi tajiri za viwanda G8 zinabidi pia zichangie anahoji bwana Morinho.

Nchi zinazoendelea zinakiri kwamba utandawazi unaweza kuleta faida,wakiruhusiwa lakini na wao pia kuingiza bidhaa zao katika masoko ya nchi za viwanda.

Cha bayana kilichopitishwa mjini Dresden ni suala kwa shirika la kazi la kimataifa ILO mawaziri wakitaka kujua kwanini azimio lililopitishwa miaka kadhaa iliyopita la kuhakikisha kiwango maalum cha malipo mpaka leo bado halitatekelezwa.Katibu mkuu wa shirika la kazi la kimataifa Juan Somavia amekiri,hana nguvu za kutosha kuweza kuwashinikiza viongozi wa taifa na serikali.

 • Tarehe 09.05.2007
 • Mwandishi Oummilkheir
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHEd
 • Tarehe 09.05.2007
 • Mwandishi Oummilkheir
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHEd
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com