1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Annapolis

Bermann,Christiana21 Novemba 2007

Mkutano wa Mashariki ya kati huko Annapolis,Marekani utafunguliwa jumaane ijayo.Mialiko imetolewa.

https://p.dw.com/p/CPwJ
President Bush mwenyeji AnnapolisPicha: AP

Mkutano wa amani juu ya Mashariki ya kati uliopangwa huko Annapolis,Maryland, Marekani jumaane ijayo unanyemelea.Wenyeji Marekani, nao wameshapeleka mialiko na miongoni mwa watakaoshiriki ni wajumbe kutoka nchi 40 na mashirika ya kimataifa.

Hata Syria na Saudi Arabia, ambazo hazina uhusiano wa kibalozi na Israel, zimealikwa kuhudhuria.

Mkutano hasa utaanza jumaane ijayo mjini Annapolis,Maryland, lakini tayari siku moja kabla hapo jumatatu, rais George Bush atakuwa na mazungumzo huko White House (ikulu) mjini Washington tangu na waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert hata na Rais wa Mamlaka ya Ndani ya wapalestina, Mahmud Abbas.

Siku hiyo hiyo,waziri wa nje wa Marekani Dr.C.Rice amewaalika kwa kikao maalumu waakilishi wa lile kundi la pande 4-UM,Russia,Marekani na Umoja wa Ulaya.

Jioni karamu maalumu itaandaliwa akihudhuria rais Bush,Dr.C.Rice na wajumbe wote wanaoshiriki katika mkutanoni.

Jumaane ijayo,siku inayofuatia, wajumbe wote walioalikwa watashiriki mkutanoni katika Chuo cha wanamaji cha Marekani huko Annapolis,si mbali sana na Washington ili kutoa mashauri yao juu ya jinsi gani ya kukifumbua kitandawili cha Mashariki ya Kati.

Isitoshe, Marekani pamoja na Palestina na Israel,wanapanga kukutana kabla hapo jumatano rais Bush kwa mara nyengine tena pekee yao na waziri mkuu Olmert na Mahmud Abbas wa Mamlaka ya ndani ya wapalestina hawakukutana Ikulu (White House).

Sean Mc Cormarc ,msemaji wa wizara ya nje ya Marekani ameasema:

“Mkutano huu, unabainisha jinsi juhudi juhudi walizochukua waziri mkuu Olmert na rais Mahmud Abbas zinavyoungwa mkono na mataifa ulimwenguni kuelekea kuundwa kwa dola la Palestina kandoni mwa lile la Israel.”

Walioalikwa huko Annapolis mbali na Israel na Palestina, ni Katibu mkuu wa UM ,Tume ya UU,Katibu mkuu wa Jumuiya ya nchi za kiarabu Arab League,Misri,Saudi Artabia,Libanon na Syria.

Bado lakini hakujapatikana majibu kutoka pande zote hizo iwapo zimeiitikia mualiko.Imefahamika kutoka ikulu, mjini Washington kwamba rais Bush amempigia simu binafsi mfalme Abdullah wa Saudi Arabia.

Kwani, kuungamkono mkutano huu Saudi Arabia ni muhimu sana ili kuzivutia nchi nyingi za kiarabu pia kuhudhuria.Hata kushiriki kwa Syria kutakua maendeleo makubwa katika juhudi kuupanua zaidi utaratibu wa amani katika mashariki ya kati.

Akielezea matumaini yake juu ya mkutano wa Annapolis wa wiki ijayo, mjumbe maalumu wa Marekani kwa Mashariki ya kati Welch alisema:

“Haikuwa rahisi kufika hapa tulipo.Pande zote mbili, zilibidi kupitisha uamuzi mgumu.Hali ya mambo lakini sasa ni nyengine kabisa kuliko ilivyokua.Inafungua njia kwa Waisraeli na wapalestina, siku moja baada ya mkutano huu, kukaa pamoja kwa majadiliano barabara.Na hii, ni muhimu kwa masilahi yetu ya kitaifa katika eneo hilo.”