1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa kupigana na njaa Berlin

10 Desemba 2008

Mkutano wa kupiga vita njaa duniani umefunguliwa Berlin.

https://p.dw.com/p/GDCx

Mjini Berlin umefunguliwa mkutano wa kimataifa china ya kichwa cha habari: "Siasa ya kupioga vita njaa".Wajumbe mkutanoni wanajadiliana wakati huu na wanapendekeza mashauri ya kuhakikisha haki za chakula kwa mwanadamu.Mkutano huu halkadhalika unatoa jukwaa la mtu binafsi kuelezea maafa yaliomfika katika shida za kujipatia chakula.mmoja kati ya wajumbe wa aina hiyo ni Mganda Peter Baleke Kayiira.

Peter Kayiira amewasili kwenye ukumbi wa mkutano huu wa 7 wa kimatifa mjini Berlin kutoka Uganda na sio tu kusimulia kisa chake binafsi kilichomfika bali kupigania haki ya mwanadamu kujipatia chakula.

Ni hadithi za watu wanaokufa na njaa na chanzo chake.Maafa ya njaa yalimsibu Kayiira na wakaazi wengine wa kiji chake hapo juni,2001 pale serikali ya Uganda walipowatimua kutoka ardhi zao ili mwanabiashara wa kahawa wa kijerumani Neumann aweze kuanzisha shamba la kahawa.

"Serikali ya Uganda ilifunga mapatano na kampuni la kahawa la Neumann mjini Hamburg.Halafu tukapewa muda wa mwisho wa kuhama -muda wa miezi 2.Hadi auguti mosi tulipasa kuondoka bila ya kujua tufanye nini kingine na hata bila ya kulipwa fidia.sisi tukapinga kuondoka.Serikali ikaleta jeshi ili kututimua.Walitumia nguvu mno kutuondosha ,tulipigwa na nyumba zetu zilitiwa moto na mali zetu ziliporwa.Na hapo tukabidi kukimbia ili kunusuru maisha yetu."alisema Peter.

Kiasi cha familia 400 zilikimbilia msituni.Zilipoteza maskani zao ,ardhi na mapato yao.Ni namna hii umasikini unapokuja na ndio hivyo njaa inavyoingia-alisema Peter Kayiira.Aliongeza:

"Kabla kutimuliwa shambani kwetu ,hali zetu zilikuwa nzuri kabisa.Tuliweza kujitoshelezea wenyewe kwa mahitaji yetu na tulikuwa hata na mazao ziyada ambayo tukiuza.Sasa mambo ni tiofauti. Sasa tuna mudu chakula mara moja tu kwa siku.

Watoto wetu hamudu tena kwenda shuleni na hali ikiendelea hivi,hatutakawia kugeuka watumwa."

Lakini Peter, amevinjari kutosalim amri na kutoridhia aliofanyiwa.Pamoja na jirani zake ameunda chama walichokiita "Simama na upiganie haki yako" .Ameishtaki serikali ya Uganda na kampuni la kahawa la mjerumani la Neumann.Mjini berlin, mbali na Peter Kayiira wamewasili wakereketwa wenzake kutoka India na Amerika ;Kusini kupaza sauti zao kwavile hata nao wanapinga kutimuliwa kwa wakaazi wa vijijini kutoka ardhi zao.Lakini hata wanasiasa,wataalamu wa sayansi na watumishi wa mashirika ya misaada wanapasa sauti zao kwenye mkutano huu mjini Berlin.

Miongoni mwao ni Olivier Schutter,mtaalamu wa sheria za kimataifa.

Yeye anaeleza kwamba 1996 kulikuwa na watu milioni 820 waliokufa na njaa ulimwenguni.Mwaka 2005 idadi yao ikafikia milioni 852 na leo hii ni milioni 975.Tunashindwa-anasema vibaya sana vita vya kupambana na njaa duniani tena katika sayari ambayo kuna chakula cha kutosha kwa wsote.

Nae waziri wa kilimo wa Ujerumani bibi Ilse Aigner,mwenyeji wa mkutano huu kwa kutimua mwaka wa 60 wa Tangazo la Haki za Binadamu ulimwenguni wiki hii, atapigania haki ya kila mtu kujipatia chakula.