Mkutano wa kilele wa Umoja wa ulaya | Magazetini | DW | 01.09.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Magazetini

Mkutano wa kilele wa Umoja wa ulaya

Bora suluhu kuliko hatua kali wanasema baadhi ya viongozi wa Umoja wa ulaya

default

Rais Medvedev wa UrusiMkutano wa chama cha mrengo wa shoto Die Linke katika jimbo la Hessen ,kumezwa Dresdner Bank na Commerzbank na mkutano wa viongozi wa Umoja wa ulaya mjini Brussels ndizo mada zilizo hanikiza magazetini nchini Ujerumani hii leo.


Tuanze lakini na mkutano wa dharura wa viongozi wa Umoja wa Ulaya kuhusu mzozo wa Caucasus.Gazeti la FRANKFURTER RUNDSCHAU linaandika: "Viongozi wa Umoja wa ulaya wanabidi wauangalie mkutano huu kua  ni fursa ya maana.Katika suala la mshikamano mara nyingi wanakua na ila.Na mara hii pia hali si nyengine.Viongozi wa nchi za Ulaya ya mashariki wanahisi hofu zao kuelekea Urusi si za bure,kwa hivyo wanawataka wenzao wa magharibi wakubali vikwazo viwekwe dhidi ya Moscow.Hatua zenyewe za kutuliza mori hazitasaidia kitu.La maana ni kama umoja wa Ulaya utafanikiwa kujipatia sifa ya mpatanishi.Usinge elemea upande wowote,si wa Urusi na wala si wa Georgia.Kwa kuhimiza juhudi za upatanishi zifanyike chini ya usimamizi wa jumuia ya Usalama na Ushirikiano barani Ulaya,Umoja wa ulaya utajipatia imani kuweza kuzileta pande zote zinazohusika katika meza ya majadiliano.Gazeti la HANDELSBLATT linahisi viongozi wa Umoja wa ulaya wanaokutana mjini Brussels wanabidi wabainishe msimamo mkakamavu dhidi ya UIrusi.Gazeti linaendelea kuandika:


"Sio tuu matamshi makali,hatua za maana pia zinahitajika.Ingekua vyema kwa mfano  kama mkutano ulioanza July iliyopita kuhusu mkataba mpya wa urafiki na ushirikiano ,ungesitishwa hadi mkutano wa kilele kati ya Urusi na Umoja wa ulaya mwezi November ujao na kuanzishwa upya baada ya hali ya mambo kupambazuka.Urusi na Umoja wa ulaya zimekubaliana katika mkataba wa urafiki,zitaheshimu misingi ya pamoja linapohusika suala la kuheshimiwa mamlaka ya taifa na kusaka ufumbuzi wa amani mizozo inapozuka.Kwa hivyo hawawezi kukaa kimya kana kwamba hakuna kilichotokea.Hata hivyo njia za mawasiliano zinabidi ziwe wazi kwa namna ambayo viongozi wa Ulaya wataweza kujibisha haraka ishara za suluhu kutoka Moscow.Magazeti ya Ujerumani takriban kwa wingi wao yameshangiria kumezwa benki ya Dresdner Bank na Commerzkbank.Gazeti la FRANKFURTER ALLGEMEINER ZEITUNG linaandika:"Ni habari za kutia moyo kwa Ujerumani.Benki hizo zilizoungana zinajiunga katika soko la fedha pamoja na Deutsche Bank.Wanaviwanda wa Ujerumani wanafurahia kuwa na benki ya pili kubwa-wengi wanapendelea kua na benki mbadala na Deutsche Bank ili kuendesha shughuli zao na ndani na nje pia.Hata kwa wateja wa kibinafsi muungano huo ni wa kutia moyo."Gazeti la DRESDNER NEUESTEN NACHRICHTEN nalo pia linahisi uamuzi wa kuungana benki hizo mbili mashuri za Ujerumani ni wa maana.Gazeti linaendelea kuandika:


"Kampuni la Allianz halijauza tawi lake kwa  benki ya Maendeleo ya China.Hakuna mfanyabiashara yeyote atakaelazimika kufungulia madaftari yake benki ya Asia ili iweze kupatiwa mikopo.Na soko la hisa la mjini Frankfurt am Main linajipatia benki ya pili kubwa inayothaminiwa hata nje ya mipaka ya Ujerumani.Hata kama ni ndogo ikilinganishwa na Deutsche Bank,hata hivyo Commerzbank kwa kuungana na Dresdner Bank imekua mara mbili.Itaweza siku za mbele kuwa na wateja wengi zaidi na kujipatia fedha nyingi zaidi.Na inajipatia uwezo wa kuingia katika nyanja nyengine pia za kibiashara.


 • Tarehe 01.09.2008
 • Mwandishi Hamidou, Oumilkher
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/F8TA
 • Tarehe 01.09.2008
 • Mwandishi Hamidou, Oumilkher
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/F8TA
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com