Mkutano wa kilele wa hali ya hewa umevunja moyo | Magazetini | DW | 21.12.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Magazetini

Mkutano wa kilele wa hali ya hewa umevunja moyo

Wahariri wanataraji hata hivyo duru ya mwakani mjini Bonn italeta tija

default

Kansela Merkel akizungumza na waandishi habari mjini Copenhagen

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani wamevunjika moyo kutokana na matokeo finyu ya mkutano wa kilele wa hali ya hewa mjini Copenhagen.Hata hivyo kuna wanaohisi matumaini bado yapo.Mbali na Copenhgagen,wahariri wameendelea na kutathmini shughuli za vikosi vya Ujerumani-Bundeswehr nchini Afghanistan.

Tuanzie lakini Copenhagen.Gazeti la "SÜDDEUTSCHE ZEITUNG" linaandika:

Copenhagen ni fadhaa kwa jumuia ya kimataifa.Watu hawajawahi kujiwekea matumaini makubwa kufuatia mkutano wa hali ya hewa kama ilivyokua safari hii-haijawahi kushuhudiwa katika historia kwamba viongozi wengi kama hivi,wa taifa na serikali wanakusanyika mahala pamoja ili kusaka ufumbuzi wa tatizo moja.Lakini tatizo hilo hawakulifumbua-wamelizidisha.Badala yake ilikua kama wanairudia filamu mbaya-wakuu wa mataifa tajiri kiviwanda wanaahidi kuanzisha fuko la misaada ili kuzituliza nchi zinazoinukia.Wametaka kujitoa kimaso maso tuu.

Ggazeti la FRANIKFURTER RUNDSCHAU halioni kama kuna haja ya kuitishwa duru nyengine ya mazungumzo.Gazeti linaendelea kuandika:

Hakuna maana ya kuendelea na duru nyengine ya sarakasi ya mkutano wa kilele wa Umoja wa mataifa kuhusu hali ya hewa.Fursa pekee iliyosalia ni kuwaachia wale waliochafua sana hali ya hewa,wawajibike zaidi-ikilazimika hata bila ya kutolewa masharti kwa nchi nyengine.Mataifa 15 ya dunia,yanabeba peke yao jukumu la kumwaga asili mia 80 ya moshi wa Carbon Dioxide ulimwenguni.Viongozi wote wa mataifa hayo wamesema jinsi hifadhi ya hali ya hewa ilivyo muhimu kwao.Kwa hivyo sasa wanabidi wawajibike na wapiga kura wao wanalazimika kuwachunguza.Na wasiwachague tena kama hawatotekeleza ahadi walizotoa.

Gazeti la WESTDEUTSCHE ZEITUNG la mjini Düsseldorf linahisi bado kuna matumaini.Gazeti linaandika:

Tamaa iko.Mwakani duru nyengine ya mkutano wa hali ya hewa itafanyika mjini Bonn.Mawaziri wa mazingira tuu ndio watakaokutana na tukimtenga mwenyeji ,kansela Angela Merkel,hakuna kiongozi mwenyegine wa taifa au serikali atakaehudhuria.Huenda duru hiyo ikaleta tija."´

Guttenberg mit Hamid Karsai in Kabul, Afghanistan

Waziri wa ulinzi zu Guttenberg akizungumza na rais Hamid Karsai

Mada yetu ya pili magazetini inahusu juhudi za wanajeshi wa Ujerumani-Bundeswehr-nchini Afghanistan.Gazeti la "Stuttgarter Nachrichten" linaandika:

Kwasababu wananchi hivi sasa wanataka kujua kwanini tunapigana vita,malengo yetu ni yepi na mhanga utakua wa aina gani ,ndiyo maana SPD wanataka wanajeshi warejeshwe nyumbani toka Afghanistan.Kawasababu hayo ndio watu wanayotaka kuyasikia,ndio wanayodai,na kusisitiza shughuli za wanajeshi wa Ujerumani -Bundeswehr nchini Afghanistan zikome.Na ilivyokua vita havina maana na vinabidi visitishwe haraka,ndio maana vikosi zaidi vinahitajika kama nchi nyengine shirika zinavyopanga kufanya:

Mwandishi:Hamidou Oummilkhheir (Inlndaspresse)

Mhariri:Abdul-Rahman

 • Tarehe 21.12.2009
 • Mwandishi Oumilkher Hamidou
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/L9lH
 • Tarehe 21.12.2009
 • Mwandishi Oumilkher Hamidou
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/L9lH
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com