Mkutano wa kilele wa Baraza la Ulaya | Habari za Ulimwengu | DW | 17.05.2005
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Mkutano wa kilele wa Baraza la Ulaya

Tangazo la kwanza la mkutano wa wakuu wa nchi na serekali 46 ziliomo katika baraza la Ulaya lilikuwa tayari limeshatiwa saini hata kabla ya kufunguliwa duru ya pili ya mashauriano. Katika tangazo hilo baraza la Ulaya na Jumuiya ya Usalama na Ushirikiano barani Ulaya zilikubaliana kushirikiana kwa njia ilio bora zaidi ili kwamba mifumo ya nguvu za Ulaya irekebishwe upya. Mchango muhimu katika shughuli hiyo itatolewa na mkuu wa sasa wa Jumuiya ya Ulya, waziri mkuu wa Luxembourg, Jean-Claude Juncker….

Rais wa Jumuiya ya Ulaya na waziri mkuu wa Luxembourg, Jean-Claude Juncker

Rais wa Jumuiya ya Ulaya na waziri mkuu wa Luxembourg, Jean-Claude Juncker

Jean-Claude Juncker, mwanasiasa anayejitambulisha sana na Umoja wa Ulaya, atapunguza misuguanoilioko baina ya Baraza la Ulaya na Jumuiya ya Ulaya. Hilo ni jukumu, kwa mujibu wa mwenyewe Juncker, ambalo atapenda kulitekeleza.

Insert: O-Ton Juncker:

+Tangu nilipokuwa mwanafunzi kijana mjini Strassbourg, kila wakati nilifuatiliza majadiliano ya hadhara ya Wabunge wa nchi ziliomo katika Baraza la Ulaya. Nafanya hivyo sasa pia. Ninapotayarisha hotuba zangu, basi mimi hutiwa moyo na ripoti za Hadhara ya Baraza la Ulaya ambazo ni nzuri sana; hizo huwa ni kiini cha mimi kutiwa moyo.+

Kwamba Bwana Juncker anatambua hayo haibadilishi ule ukweli kwamba taasisi hiyo ya Baraza la Ulaya imekwama katika mzozo wa kisiasa. Nchi wanachama wa Baraza la Ulaya, kwa mfano Ukraine, ambazo sio kati ya zile zenye mafungamano makubwa na Jumuiya ya Ulaya, kwa sehemu, zinaliona Baraza la Ulaya kuwa kama tingatinga litakalosaidia kupeleka mbele hamu za nchi hizo kuingizwa katika Jumuiya ya Ulaya.

Hivi sasa kuna malalamiko ya kimataifa dhidi ya taasisi inayobeba bendera ya Baraza la Ulaya, yaani ile mahakama ya Ulaya juu ya haki za binadamu. Kuna kesi zipatazo 8,000 za kuendewa kinyume haki za binadamu ambazo hadi sasa hazijashughulikiwa na mahakama hiyo, zimebakia katika mashubaka. Na ndio maana rais wa mahaka hiyo, Wildhaber,ametaka zichukuliwe hatua kali.

Kansela Gerhard Schroader wa Ujerumani, ambaye aliwasili leo mchana mjini Warsaw kwa ajili ya mkutano wa Baraza la Ulaya, alihakikisha kwamba baraza hilo lina umuhimu mkubwa wa kimataifa. Alisema bila ya baraza hilo, mambo hayaendi, lakini mustakbali wa taasisi hiyo unategemea uwezo wake wa kuwa tayari kujibadilisha.

Insert: O-Ton Schroader:

+ Sote kwa pamoja tujitahidi kuona kwamba kazi za Mahakama ya Ulaya ya Haki za Binadamu zinakuwa rahisi na zinaboreka. Suala jingine muhimu ni kuhakikisha kuna uhuru wa watu kutoa maoni na pia wa vyombo vya habari. Ni jukumu la Baraza la Ulaya kuweka vipimo vya mambo hayo. Hivi sasa tunahitaji kupambana na mambo matatu ambayo yamewafanya wanadamu kuwa mahabusu, nayo ni ugaidi, binadamu kufanywa kama bidhaa za biashara na mtindo wa kihalifu wa kuzichukuwa fedha zinazotokana na biashara za magendo na ulanguzi kuingizwa katika mfumo wa biashara halali.+

Masuala hayo yote matatu yatakubaliwa hii leo na nchi 46 za Ulaya na yatakuwemo katika mkataba wao utakatangzwa. Kwa mfano, kutatajwa njia zilizo bora za kupambana na mtindo wa kugharimia ugaidi kwa kutumia fedha zilizotokana na biashara za magendo na ulanguzi. Baada ya kuweko kwa muda mfupi katika mkutano huo wa kilele wa Baraza la Ulaya huko Warsaw, Kansela Schroader ameshaelekea Prague, mji mkuu wa Jamhuri ya Cheki.

Miraji Othman