Mkutano wa kilele wa Afrika na Ufaransa kuanza kesho | Matukio ya Afrika | DW | 05.12.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Mkutano wa kilele wa Afrika na Ufaransa kuanza kesho

Viongozi wa mataifa 40 ya Afrika wanakutana na Rais wa Ufaransa, Francois Hollande, mjini Paris kesho katika mkutano wa kilele wa pande hizo mbili, ambapo maudhui makuu ya mkutano huo ni usalama barani Afrika.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Bernard Membe.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Bernard Membe.

Hivi leo Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Laurent Fabius, anakutana na wenzake wa mataifa hayo ya Afrika katika mkesha wa mkutano huo wa kilele, ambao miongoni mwa nchi zinazohudhuria na zikipewa umuhimu mkubwa ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo kimsingi haina mafungamano ya kihistoria na Ufaransa. Jee kwa nini ikawa hivyo?

Mohammed Khelef amezungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Bernard Membe, ambaye alipitia Ujerumani akiwa njiani kuelekea Paris, mwanzoni mwa wiki hii.

Kusikiliza mahojiano hayo, tafadhali bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mahojiano: Mohammed Khelef/Benard Membe
Mhariri: Mohamed Abdul-Rahman

Sauti na Vidio Kuhusu Mada