1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa Jumuiya ya kiislamu Dakar

13 Machi 2008

Mkutano wa nchi 57 za jumuiya ya kiislamu umeanza Dakar ,Senegal ukilenga kuidhinisha mkataba mpya wa jumuiya.

https://p.dw.com/p/DNpX

Mkutano wa jumuiya ya nchi za kiislamu -Organisation of Islamic Conference (OIC) unaanza leo hadi kesho ijumaa mjini Dakar,Senegal ukilenga kupitisha mkataba mpya na wa kisasa ili kupiga vita itikadi kali, umasikini na kusisitiza maadili ya kuvumiliana na masikizano yanayoshikamana na didi ya kiislamu mbele ya wimbi la kampeni inayoendeshwa katika nchi za magharibi dhidi ya uislamu.

"Ikiwa tofauti za dakika ya mwisho zitasuluhishwa mkataba wa kisasa wa Jumuiya hii ya nchi 57 za kiislamu-OIC),

utaidhinishwa hapo kesho ijumaa na viongozi wa nchi hizo katika mkutano wao wa kilele.

Katibu mkuu wa Jumuiya ya nchi za kiislamu Ekmeleddin Ihsanoglu alisema,

"Mkataba huu mpya unafuata lugha ya UM kuonesha wastani na uvumilivu wa dini ya kiislamu na inalenga katika maendeleo na mshikamano baina ya wanachama wake."

Alisema hayo mwishoni mwa kikao cha mawaziri wa nje wa jumuiya hiyo.

Alisema zaidi kwamba, mageuzi katika vifungu 40 vya mkataba huo yatairuhusu Jumuiya hii ya nchi za kiislamu kuchangia zaidi katika kujipatia sauti kubwa zaidi katika ulimwengu wa kiislamu na wa utamndawazi.Ulimwengu unatanda kutoka Mashariki ya kati,Afrika hadi Asia.

Pamoja na mkakati huo ni kuhimiza ushirikiano mkubwa zaidi na misaada zaidi baina ya wanachama wake walio tajiri mfano wa Saudi Arabia na Kuweit na wale masikini hasa Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara ambako vikundi vyenye itikadi kali kama vile Al qaeda vinajitahidi kutia mizizi yake.

Jumuiya ya nchi za kiislamu imekuwa ikikosolewa mno na baadhi ya wanachama wake kwa kushindwa kutatua migogoro miongoni mwao na kwa kutotoa misaada ya kutosha pamoja na kumalizikia kulaani tu kwa mdomo hujuma za Israel dhidi ya wapalestina.

Mkataba wa sasa wa Jumuiya hii ulifungwa hapo 1972 pale wanachama wake walipogawika kutokana na mafungamano yao na pande mojawapo za vita baridi.Dola kuu na tajiri kabisa katika jumuiya hii-Saudi Arabia lilielemea Marekani wakati dola nyengine mfano wa Misri wakati ule zilikuwa na usuhuba mkubwa na Urusi.

Miongoni mwa tofauti zinazobidi kutatuliwa kabla ya kuidhinishwa hapo kesho kwa muujibu wa waziri wa nje wa Senegal Cheikh Tidane Gadio ni mizozo ya ndani ya kikabila na ya ardhi na ile na nchi jirani za kiislamu.

Rais Abdoulaye Wade anafanya jaribio jengine leo la kuwapatanisha rais Omar a-Bashir wa Sudan na jirani yake Idriss Deby wa Chad chini ya moyo huo.

Wajumbe mkutanoni mjini Dakar walitoa mfano wa Uganda, inayopinga mageuzi kwenye mkataba unaoruhusu nchi kama Uganda zisizo na wakaazi wengi zaidi wa kiislamu ,lakini zimekaribishwa kuwa wanachama.

Nyengine ni Pakistan inayoshikilia mkataba mpya utoe masharti kuwa wanachama wowote wale wapya katika Jumuiya hii kwanza wasuluhishe mzozo wao na wanachama wa sasa kabla kufunguliwa mlango wa kuingia.

Katibu mkuu Ihsanoglu alidai kwamba jamii ya waislamu inazidi kutikiswa ndani na wale wenye itikadi kali na kuandamwa katika nchi za magharibi.

Waislamu wengi wanahisi uislamu na viongozi wsake watukufu wanahujum,iwa na vyombo vya habari na wanasiasa wa magharibi chini ya kawa la kutetea uhuru wa kusema mtu atakayo.Vikatuni juu ya Mtume Muhammad vilivyochapishwa na magazeti ya ulaya vilichochea balaa kubwa na machafuko katika ulimwengu wa kiislamu 2006 na hivi karibuni ambamo si chini ya watu 50 waliuwawa.