1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa IOC wafanyika mjini Kampala,Uganda

25 Januari 2010

Wabunge kutoka nchi 51 wanachama wa Jumuiya ya nchi za Kiislamu, IOC, wanakutana mjini Kampala katika mkutano wa wiki moja, kuzungumzia changamoto zinazozikabili mataifa hayo ya Kiislamu.

https://p.dw.com/p/LgQp
Nembo ya Jumuiya ya nchi za Kiislamu,OIC

Mbali na suala la ugaidi, mkutano huo pia unapania kutafuta mkakati wa kuboresha umoja na upatanishi katika nchi wanachama. Kuimarishwa kwa elimu na kudhibiti hali ya usalama katika mataifa hayo ni miongoni mwa mada ambazo pia zitakuwa mezani. Wawakilishi katika mkutano huo wanatokea Mashariki ya Kati, Bara la Asia, Afrika na hata nchi za eneo la Balkan, barani Ulaya. Mkutano huo ulioanza jana utamalizika tarehe 31.

Leyla Ndinda kutoka Kampala ana ripoti kamili.

Mtayarishaji: Leyla Ndinda

Mhariri: Othman Miraji