Mkutano wa ANC wafunguliwa Polokwane | Habari za Ulimwengu | DW | 16.12.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Mkutano wa ANC wafunguliwa Polokwane

Polokwane-Afrika kusini:Mkutano mkuu wa chama tawala cha Afrika Kusini-African National Congress-ANC umefunguliwa mjini Polokwane.katika jimbo la Limpopo kaskazini magharibi ya nchi hiyo.Mkutano huo unapewa umuhimu mkubwa na unatazamiwa kuamua juu ya hatima ya kisiasa wa rais Thabo Mbeki.Hali ni tete na wajumbe zaidi ya elfu nne wa chama hicho kinachodhibiti uongozi wa Afrika kusini tangu enzi za ubaguzi wa rangi na mtengano zilipotoweka mnamo mwaka 1994,,wanabidi wamchague kiongozi wa chama kwa kipindi cha miaka mitano, uamuzi utakaoshawishi pia muundo wa serikali ya nchi hiyo yenye wakaazi milioni 48.Rais Thabo Mbeki anatetea tena wadhifa huo dhidi ya mpinzani wake mkubwa,makamo wa rais wa zamani Jacob Zuma.Hatima ya rais Thabo Mbeki itajulikana kesho.Katiba ya nchi hiyo haimruhusu rais Mbeki kutetea wadhifa wake wa urais kwa mara ya tatu

 • Tarehe 16.12.2007
 • Mwandishi Oummilkheir
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CcHM
 • Tarehe 16.12.2007
 • Mwandishi Oummilkheir
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CcHM

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com