1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa amani kuhusu Syria Geneva wapigwa dana dana

28 Juni 2013

Mazungumzo ya Syria Geneva, yanasogezwa mbele. Mvutano kati ya Urusi na Marekani ni jinamizi kwa baraza la usalama la umoja wa mataifa, katibu mkuu wa umoja wa mataifa ana hofu kuhusu mazungumzo hayo ya syria.

https://p.dw.com/p/18yFC
Russian President Vladimir Putin speaks at the presidential summer residence Kultaranta in Naantali, Finland on June 25, 2013. Putin is in Finland for talks on bilateral and Russia-EU issues. AFP PHOTO / LEHTIKUVA / KIMMO MANTYLA *** FINLAND OUT *** (Photo credit should read KIMMO MANTYLA/AFP/Getty Images)
Vladimir PutinPicha: Kimmo Mantyla/AFP/Getty Images

Mkutano wa hivi karibuni wa nchi G8 uliofanyikia Ireland ya Kaskazini ulitoa picha ni kwa kiasi gain mvutano kuhusu mazungumzo ya mani ya Syria umeigawa Marekani na Urusi. Mvutano huo pia ulidhihirika wazi katika nyuso za viongozi hao wawili wakiwa katika viti vyao katika mkutano huo, ambapo Obama akionekana kung'ata mdomo, huku Vladmir Putin akiinamisha uso wake chini ya ardhi.

Picha hiyo ya viongozi wawili hao imeonesha kuongezeka kwa wasiwasi katika uhusiano wa mahasimu hao wawili wa vita baridi ambao wanajikuta katika wakati mgumu kutafuta suluhisho la kadhia ngumu ikiwemo kadhia ya Syria.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry na mwenzie wa Urusi Sergei Lavrov awali walitangaza wangefanya mkutano huo uliokuwa na lengo la kuwaleta pamoja waasi na wawakilishi wa serikali ya Assad ili kufanya makubalino hadi kufikia mwezi mei mwaka huu. Lakini tarehe ya mazungumzo hayo inaonekana kupigwa dana dana, kwani awali ilikuwa mkutano huo umepangiwa kufanyika mwezi huu.

Lakini mapema wiki hii mpatanishi wa amani wa umoja wa mataifa na umoja wa nchi za kiarabu Lakhdar Brahimi, ambaye alikuwa na mazungumzo na viongozo wakuu wa Marekani na Urusi katika mkutano wa Gineva alisema mkutano huo utafanyika kabla ya mwezi Agosti mwaka huu.

Wanadiplomasia wa umoja wa mataifa kutoka Marekani wanasema haijakuwa wazi kama mkutano huo wa Syria utafanyika kweli, huku kiongozi mkuu wa wanadiplomasia hao wa magharibi akisema haionekani mkutano huo kuwa mzuri.

Nukta ya msingi katika mkutano huo ilikuwa ni kupitia mpango wa mwaka uliopita uliofikiwa mjini Geniva, ambapo katika mkutano huo Moscow na Washington zilikubaliana uwapo na serikali ya mpito ya Syria, lakini waliacha wazi suali la iwapo Rai Assad anaweza kushiriki katika mazungumzo hayo.

Obama asisitiza kutokuwapo Assad katika serikali ya mpito

Kwa upande wake Marekani na waasi wa Syria wanasema Rais Assad na familia yake hawatakiwi kuwapo katika serikali hiyo ya mpito, ingawa Urusi inasisitiza kutokuwapo kwa masharti yoyote katika mazungumzo hayo.

URais Barack Obama
Rais Barack ObamaPicha: Reuters

Kuna nukta zingine za kuzingatia katika majadiliano ya kile walichokiita wanadiplomasia wa umoja wa mataifa "Geneva 2",kufanyika mkutano huo ukiwakilisha utawala wa Assad na wapinzani wa Syria katika meza ya mazungumzo.

Hadi sasa hakuna makubaliano yoyote ya kupanga watu mhimu wa kushiriki katika mazungmzo hayo lakini pia suala la uwezekano wa kushiriki washirika wengine Assadi mfano Iran kama ambavyo Urusi inasisitiza Iran kuwapo katika mazungumzo hayo licha ya Marekani kupinga hilo.

Mwanadiplomasia huyo anasema ni vyema kuwafanya wapinzani na utawala wa Assd kukubali kukaa pamoja katika mazungumzo ya Geniva, hasa katika hali ambayo Rais Assad anafikiria atashinda vita hiyo kwa nguvu za jeshi huku waasi nao wakishkilia nukta ya udhaifu wao wakiomba msaada zaidi wa silaha.

Wanadiplomasia hao wa umoja wa mataifa wanasema katibu mkuu wa umoja huo Ban Ki-moon ambaye yupo katika kipindi chake cha mwisho cha uongozii ana hofia kuwa anaweza kukumbukwa kama kiongozi aliyeshindwa kumaliza matatizo ya Syria.

Awali wiki hii Wazri wa mambo ya nje wa Rais Assad Walid al-Moualem, aliwambia waandishi wa habari serikali ipo tayri kuunda serikali ya umoja wa kitaifa, lakini amesisitita hawana mpango wa kuachia madaraka nchini Syria.

Richard Gowan wa chuo kikuu cha New York ametabiri kuwa, kushindwa kwa mkutano huo unaosimamiwa na Kerry, utaongeza shinikizo kwa rasi Obama kutumia njia yake ya sasa ya kutuma silaha nyingi kwa waasi wa Syria.

Mwandishi:Hashim Gulana/RTRE

Mhariri: Yusuf Saumu