1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa Afrika wa Tabianchi wafunguliwa DR Congo

Amina Mjahid
3 Oktoba 2022

Mawaziri wa mazingira kutoka mataifa takribani 50 wanakutana katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, kwa ajili ya kikao cha utangulizi wa mkutano wa kilele wa COP27.

https://p.dw.com/p/4HgqQ
USA | Kohlekraftwerk
Picha: Branden Camp/AP Photo/picture alliance

Katika Mkutano huo wa COP27, mataifa tajiri yanatazamiwa kuwekewa shinikizo kuongeza matumizi ili kuzuwia mabadiliko ya tabianchi.

Mawaziri wa mazingira kutoka mataifa takribani 50 wanakutana katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo hii leo, kwa ajili ya kikao cha utangulizi wa mkutano wa kilele wa COP27, ambapo mataifa tajiri yanatazamiwa kuwekewa shinikizo kuongeza matumizi ili kuzuwia mabadiliko ya tabianchi.

Soma zaidi: Mataifa tajiri yaahidi fedha za kuisaidia Afrika kukabiliana na tabianchi

Mazungumzo hayo yanayofanyika mjini Kinshasa siyo rasmi lakini yanakusudiwa kuyaruhusu mataifa mbalimbali na mashirika ya mazingira kufanya tathmini ya misimamo ya kisiasa kuelekea mkutano wa kilele wa COP27, utakaofanyika nchini Misri mwezi ujao.

Hafla ya ufunguzi ilitarajiwa kufanyika katika jengo la bunge la Congo mjini Kinshasa, ikifuatiwa na majadiliano juu ya kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi, na kutoa ufadhili kwa mataifa yalioharibiwa tayari na ongezeko la joto la dunia na matukio mabaya ya hali ya hewa.

Chanzo: afp