Mkutano mkuu wa umoja wa mataifa kujadili malengo ya milenia | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 21.09.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Mkutano mkuu wa umoja wa mataifa kujadili malengo ya milenia

Mkutano maalum wa umoja wa mataifa juu ya malengo ya maendeleo ya milenia unaendelea mjini New York, ambapo viongozi wa nchi na wakuu wa serikali zaidi ya 100 wanatathmini hatua iliyofikiwa.

default

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon akihutubia baraza kuu la umoja wa mataifa.

Mkutano maalum wa umoja wa Mataifa juu ya malengo ya maendeleo ya Milenia unandelea mjini New York, ambapo viongozi wa nchi na wakuu wa serikali zaidi ya 100 wanatathmini hatua iliyofikiwa hadi sasa katika kuyatekeleza malengo hayo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amesema licha ya viunzi vilivyopo njiani malengo hayo yanaweza kufikiwa katika muda unaokusudiwa yaani mwaka wa 2015.Lakini haitakuwa sawaa kusema kwamba nyana zote za malengo hayo yanaeelezwa kwa mujibu wa ratiba. Na ndiyo sababu kwamba katibu Mkuu Ban amesema muda unayoyoyoma kwani imebakia miaka mitano tu hadi kufikia mwaka wa 2015. katibu mkuu ameitaka jumuiya ya kimataifa isimame pamoja katika juhudi za kuondoa umasikini wa kusikitisha katika sehemu fulani za dunia.

Kwa kuzingatia utambulisho wetu kama jumuiya ya kimataifa iliyoundwa kutokana na katika misingi ya mshikamano , na kwa kuzingatia wajibu wetu lazima tuukomesha umasikini mkubwa wa kudhalilisha."

Hatahivyo imetiliwa maanani kwamba fedha zilizoahidiwa kwa ajili ya harakati za kupambana na umasikini zinakwenda kwa taratibu mno hasa katika nchi zinazoendelea ikiwa ni pamoja na barani Afrika kusini mwa jangwa la Sahara, sehemu inayozingatiwa kuwa yenye matatizo makubwa.Lakini rais wa Benki ya Dunia Robert Zoellick amesema Afrika inapaswa kuchukuliwa kama mdau na siyo kama kigezo cha kuamrishwa cha kufanya.Rais wa Benki ya dunia amesema Afrika ni eneo la kuvutia kwa wawekezaji vitega uchumi.

Ujerumani pia imesisitiza busara ya kuwaunga mkono wale wenye mipango ya kutekeleza utawala bora.

Akifafanua hayo Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ameeleza kuwa ni zile nchi zilizotayarisha zenyewe mipango ya kupambana na umasikini ambazo zitapewa fedha.Bibi Merkel amesema,nchi itakayopewa fedha na kuungwa mkono ni ile tu iliyoandaa yenyewe mipango juu ya kupambana na umaskini na mipango ya maendeleo. Huo ndio msingi utakaotuwezesha kushirikiana na nchi nyingine.

Lakini waziri mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi ametahadharisha kwamba baadhi ya mikakati inayofanikiwa katika sehemu nyingine haiwezekani katika sehemu fulani.

Zenawi ametoa mfano wa sekta ya afya.Wakati mwingine, kwa mfano, tunaelekeza juhudi zetu katika kutoa huduma za afya mahospitalini-jambo linalogharimu fedha nyingi.Lakini mara nyingi hospitali zipo hasa mijini. Lakini asilimia 70 ya watu nchini Ethiopia wanaishi katika sehemu za mashambani."

Katika kuhimiza juhudi za kuukabili umasikini duniani rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa amesema pana haja ya kubuni mikakati mipya katika harakati za kupambana na umasikini.Amesema baada ya kuondokana na mgogoro wa uchumi nchi haziwezi kuendelea kufuata sera zile zile. Na ndiyo sababu rais huyo wa Ufaransa amependekeza kuyatoza mabenki kodi ,na kutenga fedha zitakazopatikana kwa ajili ya kusaidia mipango ya maendeleo.

Mwandishi/Bergamann Christina./New York/

Tafsiri/Mtullya Abdu/

Mpitiaji/..... Sekione Kitojo

 • Tarehe 21.09.2010
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/PI1X
 • Tarehe 21.09.2010
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/PI1X
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com