1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano mkuu wa China wamalizika

Sekione Kitojo22 Oktoba 2007

Hakuna mkutano wa chama ambao umekuwa ukitupiwa macho na jumuiya ya kimataifa kama mkutano wa hivi karibuni wa chama cha Kikomunist cha China. Sio tu kwamba chama hiki ambacho kinawanachama milioni 73 kuwa ni chama kikubwa kabisa duniani, lakini pia ni kutokana na kushika madaraka kwa muda wa miaka 58 katika nchi hiyo kubwa kabisa , na kudhibiti bunge na sekta ya sheria pamoja na kufanikiwa kuupandisha juu uchumi wa nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/C7ge
Waziri mkuu Wen Jiabao akipunga mkono wakati wa kuwatambulisha wajumbe wa kamati kuu ya chama mjini Beijing.
Waziri mkuu Wen Jiabao akipunga mkono wakati wa kuwatambulisha wajumbe wa kamati kuu ya chama mjini Beijing.Picha: AP

Nani aliweza kudhani , kuwa chama hiki cha kikomunist nchini China kinaweza kutoa madaraka yake kwa mapenzi yake na kuiingiza nchi hiyo katika mfumo wa vyama vingi, ni dhahiri baada ya mkutano huu mkuu wa chama, kwa mara nyingine tena watakuwa wamevunjika moyo. Mkuu wa nchi na mwenyekiti wa chama Hu Jintao amesema katika hotuba yake ya ufunguzi iliyochukua saa mbili na nusu , kuwa bila shaka chama hicho kitakuwa mwakilishi pekee katika nchi hiyo. Ni kweli kwamba kila mara mtu ameweza kusikia neno Demokrasia. Shirika rasmi la habari nchini humo Xinhua limehesabu mara 60 katika hotuba ya Hu Jintao akilisema neno hilo.

Kwa mapenzi yake demokrasia ni lazima kwanza iwemo katika chama na baadaye ndipo itawezekana kupatikana msingi wa chama.

Lakini pia katika mkutano huo wa chama kumekuwa na aina fulani ya majaribio ya demokrasia. Wajumbe zaidi ya 2,200 katika mkutano huo hawakuingia katika mkutano huo kama wajumbe waliochaguliwa, lakini wapo wajumbe asilimia 15 ambao wamechaguliwa.

Katika uchaguzi wa kamati kuu siku ya Jumapili vilibaki viti 200 vya kuchaguliwa ambavyo ni asilimia 8.3. Leo Jumatatu kamati hiyo mpya inakutana kwa kikao chake cha kwanza, ili kuweza kuwachagua wajumbe hao wa kamati.

Kutokana na kustaafu kwa wajumbe watatu na mjumbe mmoja kufariki dunia , viti vinne katika kamati hii yenye madaraka makubwa nchini humo viko wazi. Mbili kati ya nafasi nne hizo mpya ni lazima ziangaliwe kwa ajili ya siku za usoni, Li Keqiang, katibu mkuu wa chama kutoka katika jimbo la Liaoning na Xi Jinping, katibu mkuu wa chama kutoka mji wa Shanghai.

Mmoja wao ni mwakilishi wa tawi la vijana wanaomzunguka mwenyekiti wa chama Hu Jintao na mwingine anaongoza lile kundi la viongozi wa kesho ambao ni watoto wa viongozi walioko madarakani hivi sasa. Kwa utaratibu wa chama Hu Jintao , ambaye tayari amechaguliwa kukiongoza chama kwa miaka mingine mitano, amethibitishwa katika wadhifa huo, na waziri mkuu Wen Jiabao , ambaye anashika nafasi ya pili katika madaraka ya nchi hiyo , kupitia uchaguzi katika kamati kuu, inaonekana nafasi yake kuwa salama, kwa muda wa miaka sita ya madaraka.

Mtu atakayechukua nafasi yake iwapo atajiuzulu bila shaka ni Li Keqiang mwenye umri wa miaka 52 ama Xi Jinping mwenye umri wa miaka 54.

Kwa demokrasia China inaweka matumani makubwa kwa wajumbe wa kamati hii kuu. Li Keqiang amesoma katika chuo kikuu cha Peking, chuo pekee cha kiliberali nchini China , amesomea sheria na kuchukua shahada ya udaktari katika masuala ya uchumi.

Akiwa kama mwenyekiti wa chama cha wanafunzi , alikuwa mtu muhimu katika kusukuma majaribio ya demokrasia katika chuo hicho kikuu mjini Peking. Hata baada ya kuingia madarakani na kupigwa msasa kisiasa , anaonekana kuwa tumaini la nguvu za mageuzi na msomi anayependelea demokrasia. Kwa kijana mwingine katika kamati hiyo kuu, Xi Jinping, ambaye ana shahada ya udaktari katika masuala ya sheria, ana mahusiano mazuri hususan na mataifa ya nje. Waziri wa fedha wa Marekani Henry Paulson anamuhesabu kama rafiki wake wa karibu.