1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano kati ya viongozi wa Urusi na Ujerumani mjini Wiesbaden

14 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Fs

Wiesbaden:

Rais Vladimir Putin wa Urusi anaanza ziara ya siku mbili nchini Ujerumani hii leo ambapo amepangiwa kuzungumza na kansela Angela Merkel.Mkutano huu wa Wiesbaden kati ya viongozi hao wawili,wakihudhuria pia mawaziri kadhaa wa nchi hizi mbili,ni sehemu ya mazungumzo ya kawaida yanayofanyika kila mwaka kati ya serikali za nchi hizi mbili.Mazungumzo ya mwaka huu yanatazamiwa kumulika mpango wa Marekani wa kuteka kinga ya makombora katika jamhuri ya Tcheki na Poland.Kansela Angela Merkel alisema hapo awali,Ulaya haistahiki kuzozana katika suala hilo.Mustakbal wa Kosovo pia ni miongoni mwa mada zitakazojadiliwa huko Wiesbaden. Hii itakua mara ya mwisho kwa rais Putin kuhudhuria mkutano kama huu kabla ya wadhifa wake kumalizika.Mikutano ya kawaida kati ya serikali za Ujerumani na Urusi imeanzishwa mwaka 2001 na kansela wa zamani Gerhard Schröder.