1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano kati ya Umoja wa ulaya na Iran kuhusu mradi wa kinuklea wa Teheran umeakhirishwa

27 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBxl

TEHERAN:

Iran na Umoja wa ulaya wameakhirisha mkutano uliokua ufanyike wiki hii kati ya muakilishi mkuu wa siasa ya nje wa Umoja wa ulaya Javier Solana na mkuu wa tume ya Iran katika mazungumzo ya kinuklea Ali Laridjani.Kwa mujibu wa msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za nje mjini Teheran,pande hizi mbili zimekubaliana kwa pamoja kuakhirisha mazungumzo hayo.Duru za kuaminika kutoka Iran zimesema wanasiasa hao wawili walikua wakutane alkhamisi ijayo nchini Hispania,kujaribu kusaka ufumbuzi wa mzozo uliosababishwa na mradi wa kinuklea wa Iran.